VIJANA katika kata za kata za Saza na Mbangala Wilayani Songwe Mkoani
Songwe wameyakimbia makazi yao na kwenda kuishi porini wakikwepa amri
ya Mkuu wa wilaya ya songwe, inayowataka vijana wote wa kata hiyo kuanza
mafunzo ya mgambo kwa nguvu, wakidai hawakushirikishwa .
Hatua ya kukimbia makazi yao na kuziacha familia zao na kwenda kuishi
porini kwa vijana hao kunadaiwa kumetokea baada ya Mkuu wa Wilaya ya
Songwe Samuel Jeremiah kutoa amri ya kuwataka vijana wote wenye umri wa
miaka kati ya 18 na 35, kuanza mafunzo ya mgambo kwa nguvu, hali ambayo
imesababisha maisha ya vijana hao pamoja na familia zao kuwa mashakani.
Vijana hao ambao ni wachimbaji wadogo wa madini na kipato chao kikiwa
kinategemea uchimbaji wa madini ili kujikimu kimaisha kumesababisha
athari kubwa katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo kuathiri
maisha ya wakazi wote wa kata hizo.
Channel ten ikapiga hodi hadi ofisi za Mkuu wa Wilay aya Songwe
Samuel Jeremih akasema suala la mafunzo ya mgambo siyo la hiari kwa
sababau ni kwaajili ya usalama wa Taifa .
Post a Comment
karibu kwa maoni