Mpango
amewataja watumishi hao kuwa ni pamoja na Harrison Mwampashi, John Makorere,
Stephene Josia na Frank Kessy na kuviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama
mpakani hapo viwahoji huku wakiwa wamesimamishwa kazi.
Watumishi
hao wanadaiwa kuiba lakiri hizo kumi kutoka ofisi za TRA-Tunduma
wanakofanyiakazi, ambapo 4 kati ya hizo lakiri zilikutwa zimefungwa kwenye
mizigo ya malori yanayoshikiliwa katika mpaka huo baada ya uchunguzi kufanyika
huku malori mengine 5 yakizuiwa baada ya kuonekana lakiri zao zimechezewa.
Taarifa
zinasema kuwa baada ya uchunguzi, mawakala ama wamiliki wa malori hayo wamedai
walipewa lakiri hizo na watuhumiwa na kwamba uchunguzi zaidi umebaini kuwa
kiwango cha mizigo kilichomo kwenye makontena yaliyobeba mizigo ya magogo na
kufungwa lakiri hizo za wizi hakilingani na idadi ya mizigo iliyoko kwenye
nyaraka jambo linaloashiria kuwa wanazitumia lakiri hizo kudanganya idadi na
uzito wa mizigo yao ili kukwepa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.
“Hakuna
kitu muhimu kama uadilifu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato na hatutasita wala
hatutamwonei aibu mtu yeyote, tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda
fedha za umma” alionya Dkt. Mpango
Alisema
kuwa Serikali imebaini baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato na Idara za
Forodha mipakani wanashirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuingilia
mifumo ya kukusanyia mapato, kitendo ambacho kinaweza kurudisha nyuma juhudi za
serikali kuwahudumia wananchi wake.
Dkt.
Mpango amewaonya wafanyakazi wote wa forodha na Mamlaka ya Mapato nchini, kuwa
wazalendo na waaminifu katika kukusanya mapato ya Serikali na kuacha
kujihusisha na vitendo vinavyokwaza ufanisi wa Mamlaka hayo.
BIASHARA
YA KUBADILISHA FEDHA MPAKANI
Wakati
huo huo, Dkt. Mpango, ametoa muda wa siku thelathini, kwa wanaobadilisha fedha
za kigeni kiholela mipakani, waache mara moja, badala yake waheshimu sheria za
Nchi, na kuunda vikundi vinavyoweza kuanzisha maduka ya kubadilisha fedha hizo.
Alitoa
kauli hiyo Mjini Tunduma, wakati akizungumza na wabadilisha fedha mpakani humo,
kwamba serikali itawaheshimu tu wale watakaojiundia vikundi na kuwa na sehemu
wanakoweza kubadilisha fedha kwa kufuata utaratibu na wala si vinginevyo.
ATEMBELEA
UJENZI WA KITUO KIPYA CHA FORODHA NA IDARA YA FORODHA TUNDUMA
Akiwa
Mjini Tunduma, Dkt. Mpango, pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua
maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpaka kati ya Tanzania
na Zambia Mjini Tunduma.
Pia
ametembela Ofisi ya Idara ya Forodha mpakani hapa, na kupata taarifa ya
makusanyo ya mapato kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, ambapo maafisa wamekusanya
mapato zaidi ya Bilioni 75 na kuvuka lengo la mapato waliyokuwa wameyatarajia.
Meneja
wa Idara ya Forodha mikoa ya Mbeya na Songwe, Bw. Jimmy Nsindo amesema kuwa
pamoja na mafanikio hayo, Mpaka huo wa Tanzania na Zambia, ni mpaka unaoweza
kuingilika kirahisi, matokeo yake udhibiti wa mapato unaingia dosari, huku
baadhi ya watanzania wanafanya biashara zinazodaiwa kuliingizia hasara taifa,
zikiwemo za kubadili fedha za kigeni kwa mfumo usio rasmi.
ASHITUKIZA
VITUO VYA MAFUTA
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa muda wa siku ishirini kwa
wamiliki wote wa vituo vya mafuta ambao wameomba kupatiwa mashine za
Kielectroniki kwaajili ya kuunganishwa na mfumo wa kodi na utoaji wa risti wawe
wamepata mashine hizo vinginevyo watafungiwa vituo vyao.
Aidha,
amesema ifikapo Jumatano Juma lijalo wamiliki wote wa maduka mkoani Mbeya,
waanze kutumia mashine za Kielekroniki za kutolea risiti (EFDs) na kuonya
kwamba Serikali haitasita kuyafunga maduka yao wasipotekeleza maagizo hayo.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.