Serikali ya
Marekani imetiliana saini na Tanzania makubaliano ya kuipatia ruzuku ya Dola za
Marekani milioni 225 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 550 kwa ajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kijamii katika sekta za afya, elimu
ya msingi, kilimo, maji na usafi wa mazingira.
Tukio hilo
limefanyika Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam ambapo
Tanzania imewakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na kwa
upande wa Serikali ya Marekani, makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID), Bw. Andy Karas
Utiwaji
saini wa makubaliano hayo umefanyika siku moja baada ya Marekani kupitia Kaimu
Balozi wake hapa nchini, Dkt. Inmi Patterson kukutana na Mhe. Rais Dkt John
Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumhakikishia kuwa Serikali yake
iko tayari kuongeza misaada kwa Tanzania.
Maeneo
ambayo fedha hizo zitatumika na kiwango chake kwenye mabano ni mapambano dhidi
ya Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (Dola milioni 98.2), Malaria (Dola milioni 46),
Kifua Kikuu (Dola milioni 5), Uzazi wa Mpango (Dola milioni 26.4), Sekta ya Kilimo
(Dola milioni 45), Maji na Usafi wa Mazingira (Dola milioni 9) na Elimu ya
msingi (Dola milioni 13.9)
Akizungumza
wakati wa tukio hilo lililohudhuriwa pia na Kaimu Balozi wa Marekani hapa
nchini Dkt. Inmi Patterson, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto
James, ameishukuru Marekani kwa msaada huo unaolenga kusadia juhudi za Serikali
za kuboresha maisha ya wananchi wake.
“Marekani
ni rafiki yetu na mdau wetu mkubwa wa maendeleo wa siku nyingi na
ninachowaahidi ni kwamba tutatupa jicho kali kuhakikisha kuwa fedha hizi
zinatumika kama ilivyokusudiwa na jinsi tulivyokubaliana” Alisisitiza Bw. James
Nae Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani kwa ujumla wanafurahishwa na hatua kubwa ya kimaendeleo iliyopigwa na Tanzania na kuahidi kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano huo kwa faida ya nchi hizo mbili.
Post a Comment
karibu kwa maoni
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.