0
 
Tiketi za kushuhudia mpambano wa masumbwi kati ya Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor ilikuwa ni dola 150,000.
Ndo Mpambano  wa gharama zaidi kuwahi kutokea na tiketi kwa sasa ziliuzwa kama njugu.
Ulifanyika  Agosti 26 katika uwanja wa T-Mobile mjini Las Vegas.
Mayweather mwenye miaka 40 awali alistaafu lakini amerejea kupambana na McGregor.
Conor McGregor sasa anasema kuwa refa Robert Byrd alifanya makosa kusimamisha pigano lake dhidi ya Floyd Mayweather katika raundi ya kumi.
Bingwa huyo wa UFC alipigwa katika pigano lake la kwanza la kulipwa huku Floyd Mayweather akiimarisha rekodi yake ya kutoshindwa hadi 50-0.
Raia huyo wa Ireland ambaye amesema atarudi kuendelea na mchezo wake wa UFC licha ya kusema huenda akarudi tena katika ulingo wa ndondi anasema kuwa alikuwa amechoka kiasi.
''Nilidhani pigano hili lilikaribia kuwa sawa, niliyumba yumba kiasi nilipochoka'',alisema.
''Refa angewacha pigano liendelee na kumruhusu Mayweather kuniangusha'' .
''Nilikuwa najua nilichokuwa nikifanya.raundi mbili za mwisho nilitaka nione kama anaweza kuniangusha.Nilidhani ilikuwa mapema mno kwa refa kusimamisha pigano hilo.Nilitaka kuendelea hadi raundi ya mwisho'', alisema

Mayweather: Sitopigana tena, lakini nikipata fursa ya kujipatia $300m kwa dakika 36 nitarudi.

 Mayweather amesema kuwa iwapo atapata fursa ya kujipatia $300m katika dakika 36 atarudi.Bondia Floyd Mayweather amesema kwamba hataonekana tena katika ulingo wa ndondi baada ya kumshinda Conor McGregor katika pigano lililomalizika kwa njia ya knockout katika raundi ya 10.
Hatahivyo Mayweather amesema kuwa iwapo atapata fursa ya kujipatia $300m katika dakika 36 atarudi.
''Mimi sio mjinga, iwapo kutakuwa na fursa ya kutengeza dola $ 300m katika dakika 36 nitarudi kupigana''.
Mayweather ambaye alistaafu baada ya kumshinda Andre Berto mnamo mwezi Septemba 2015 amesema kuwa hakuna kilichosalia kudhihirishia ulimwengu.
Aliongezea Kuwa: Hili ni pigano langu la mwisho hamutaniona tena.Mtu yeyote anayetaka kupigana nami asahau.Najiandaa kuwa mkufunzi wa ndondi ili kuwasaidia mabondia.
Mayweather alikiri kwamba pigano dhidi ya McGregor lilimchukua muda mrefu kumsimamisha mpinzani wake zaidi ya walivyodhania yeye na babake.
''Nilifanya kile ninachoweza kufanya'', alisema. ''Nilipata njia ya kumnasa na kufanikiwa kumpiga.Babangu alidhani kwamba nitamsimamisha katika raundi ya saba ama hata sita''.
''ilituchukua muda mrefu lakini hatimaye tulifanikiwa kufanya kile tunachoweza kufanya''.
Wakati wa pigano hilo Mayweather alionekana kukasirishwa na hatua ya McGregor kumpiga kisogoni.
''Nilimwachia refa kufanya kazi yake,alisema.Siko hapa kumshutumu refa lakini muliona kilichokuwa kikiendelea''.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top