Serikali imesema imeandaa kanuni kwa ajili ya kuunda mabaraza ya vijana ambayo yatawawezesha kutambua majukumu yao, kuweka mazingira mazuri ya ushirikishwaji na kushiriki katika maanuzi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akifungua mkutano wa vijana kuhusu afya na maendeleo ulioandaliwa na shirika la Save the Children.
Mhagama amesema kanuni hizo ziko tayari hivyo, kwa sasa wanaanda utaratibu wa namna ya kuunda mabara hayo ambayo yatakuwa kuanzia ngazi za Mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa ambayo yatawapa vijana fursa ya kuwasilisha mawazo yao.
Sheria ya Mabaraza ya Vijana ina lengo la kuwezesha vijana kutambua majukumu yao, kukuza na kuhimiza maadili mema, kuweka mazingira mazuri ya ushirikishwaji na ushirikiano katika kutekeleza masuala yanayohusu maendeleo ya vijana katika ngazi ya kitaifa na kimataifa
Post a Comment
karibu kwa maoni