0
Responsive imageMkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na sheikh mkuu wa Tanzania mufti Abubakar Zubeir, alipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya bakwata.
katika mazungumzo yake IGP Sirro amemuhakikishia sheikh mkuu kuwa, jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na viongozi wa kidini katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kihalifu na wahalifu hususani katika maeneo ya kuabudia.
kwa upande wake Sheikh mkuu wa Tanzania mufti Abubakar Zubeir, amesema kuwa, ili jamii iendelee kuishi kwa amani na utulivu ni vyema wakashirikiana na vyombo vya dola katika kubaini na kutanzua uhalifu uliopo katika jamii.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top