Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka na kusema kuwa wao kama
viongozi watamsifu Rais pale anapofanya vizuri hadharani na kusema
anapokosea lakini amedai hawawezi kumdhihaki Rais wala kusema mambo ya
uongo dhidi yake.
Lema
alisema hayo jana katika mkutano wake wa tisa jimboni kwake kwenye Kata
ya Sekei Sanawari, Arusha Mjini na kusema anashangazwa na watu ambao
wanasema Rais hatakiwi kusemwa hadharani.
"Sitaongea
uongo hadharani na sipo hapa kumdhihaki Rais ila Rais akikosea
nitamsema na sitamsema chumbani bali nitamsema hadharani, habari ya nchi
inavyoendeshwa tunasema hadharani, Rais akikosea tutamsema hadharani na
akipatia tutampongeza hadharani" alisema Godbless Lema
Aidha
Mbunge Lema aliendelea kutoa lawama zake kwa viongozi mbalimbali wa
dini akisema kuwa wamekuwa wakifumbia macho mbalimbali ambayo
yanaendelea ndani ya nchi hivyo ameahidi kuwa akimaliza mikutano yake
atakuja kufanya mikutano mingine kuhamasisha wanachi wasitoe sadaka kwa
taasisi za dini kwa kuwa viongozi hao wamekuwa wakifumbia macho na
kushindwa kusema juu ya ukiukwaji wa sheria ndani ya nchi na namna
ambavyo Demokrasia imekupwa ikiminywa.
Mbali
na hilo Lema alisema anawashangaa watu wanaosema kuwa Mwanasheria wa
CHADEMA Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa ameweza kusema kuwa kuna
ndege ya Tanzania imeshikiliwa nchini Canada.
"Leo
Lissu anakamatwa kwa sababu ya kusema ndege ya Tanzania imekamatwa kwa
kuwa tunadaiwa Ulaya, Polisi wanamchukua Lissu na kwenda kumsachi kwake,
mnatafuta ndege chumbani kwa mke wa Tundu Lissu, wanasema Lissu si
mzalendo sasa nani mzalendo aliyesema tunadaiwa Ulaya au aliyetaka
kuchukua fedha kinyemela akalipe deni Ulaya" alihoji Godbless Lema
Post a Comment
karibu kwa maoni