KUNDI la wasichana mjini Kisumu, Magharibi mwa Kenya wameungana na kuunda programu tumishi, yaani app, kwa jina iCut, ili kusaidia kudhibiti ukeketaji.
Wasichana hao watano ni Stacy Owino, Cynthia Otieno, Purity Achieng, Mascrine Atieno na Ivy Akinyi, walisema kwa nyakati tofauti kuwa wasichana wengi hawana ufahamu kuhusu ukeketaji na madhara yake hivyo wameamua kuandaa program hiyo kuwapa elimu kuhusu uketetaji.
Wasichana hao sasa wameteuliwa kushindania tuzo mjini San Francisco, California na wamesema kuwa ikiwa watafanikiwa watatumia pesa hizo kuboresha app hiyo na kuwasaidia wasichana walioathiriwa na ukeketaji.
Nchini humu wasichana wengi wamejikuta wakiumia kutokana na ukeketaji unaoendelezwa na baadhi ya makabila yasiyotaka kubadilika. Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa kumekuwa na mwamko miongoni mwa baahi ya wasichana wanaopata elimu, hali inayowafanya watoe taarifa kwa vyombo vinavyopinga ukeketaji pindi wanapotakiwa kukeketwa
Post a Comment
karibu kwa maoni