
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipakwa
majivu wakati wa ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu
Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana
na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya
Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma.
Magufuli
akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika
ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa
Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo
Februari 14, 2018.

Rais
John Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali
Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini wengine
katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu Joseph
jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.

Mama
Janeth Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali
Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam baada ya kujiunga na waumini
wengine katika ibada ya Jumatano ya Majivu katika kanisa la Mtakatifu
Joseph jijini Dar es salaam asubuhi ya leo Feb 14.
Post a Comment
karibu kwa maoni