Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 23 Agosti, 2017 amemteua Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi
kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya.
Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi anachukua nafasi ya Bw. Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Polisi.
Uteuzi wa Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi unaanza mara moja.
Wakati
huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Kuzuia na Kupambana na Dawa Kulevya Bw. Rogers William Siyanga ambaye
amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na
matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.
Bw.
Rogers William Siyanga amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa
na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni
bangi, heroine, cocaine, kemikali bashirifu na kwamba kwa sasa imeanza
kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.
Amebainisha
mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa
ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za
msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za
kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya, na pia
ametoa wito kwa watu wenye waathirika wa dawa za kulevya kuwapeleka
katika mamlaka hiyo ili watibiwe.
Post a Comment
karibu kwa maoni