VIDEO:POLISI WATOA RIPOTI YA KULIPULIWA KWA OFISI YA MAWAKILI
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini,
wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS),
kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la
mlipuko, uliotokea kwenye ofi si za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa
kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na kituo hiki Profesa Juma alisema TLS hawana haki ya kutoa
agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa
kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake.
Profesa Juma alisema uhuru wa mahakama ni pamoja na kuheshimu mamlaka
nyingine za nchi zinapokuwa zinafanya kazi zake. Alisema kwa kuwa tukio la
kulipuliwa kwa ofisi za Mawakili wa Immma ni tukio la kihalifu, hivyo
wanasheria waiache Polisi na vyombo vingine vya upelelezi kufanya kazi yao.
Kauli ya Jeshi la Polisi Kwa upande wao, Jeshi la Polisi limesema liachwe
liendelee na kazi ya uchunguzi, badala ya kulihusisha na tukio hilo. Msemaji wa
Jeshi hilo Makao Makuu, Kamishina Msaidizi Barnabas Mwakalukwa alisema Jeshi la
Polisi ndicho chombo chenye mamlaka ya kufanya uchunguzi na hivyo kama kuna mtu
yeyote mwenye taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, anatakiwa kuzitoa polisi badala
ya kuzungumza na vyombo vya habari.
Kauli hizo za Polisi na ya Kaimu Jaji Mkuu, zimekuja baada ya Rais wa TLS,
Tundu Lissu kuwaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Baraza lao la
Uongozi lina taarifa kuwa kikundi cha watu wenye silaha za moto, wakiwa
wamevalia sare za Jeshi la Polisi, kiliwateka nyara walinzi binafsi wa Kampuni
ya IMMMA na kuingia ndani ya eneo la ofisi hizo.
Lissu alidai watu hao baada ya kuingia ndani, walitega milipuko na madumu
manne ya mafuta ya petroli katika maeneo kadhaa ya jengo la ofisi hizo. Alidai
muda mfupi baadaye, milipuko hiyo ililipuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa
jengo la ofisi za IMMMA Advocates zilizoko Upanga pamoja na majengo jirani.
Post a Comment
karibu kwa maoni