Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amesema ataanzisha zoezi la
kupita shule kwa shule na kupiga kura ili kubaini walimu wanaotembea na
wanafunzi na kuwaharibia maisha yao ili wachukuliwe hatua stahiki.
Bi
Msafiri ametoa salamu kwa baadhi ya shule ambazo waalimu wameacha
kufundisha watoto na badala yake wamewageuza ndiyo wake zao huku akisema
kuwa atawaagiza Wakurugenzi wake kupita katika shule mbalimbali
kupigisha kura ili kuwabaini waalimu wanaofanya uharibifu huo kwa
wanafunzi kisha baadae kuwatelekeza.
Kwa upande wa Afisa elimu Mkoa wa
Njombe, Halfani Masuila, amekemea vitendo vya mahusiano baina ya
wanafunzi na walimu na kusema kuwa serikali itamchukulia hatua kali
mwalimu wa kike au wakiume atakayebainika kuwa na uhusiano na
mwanafunzi.
Bw. Masuila amesema amebaini hilo katika
shule nyingi zenye kidato cha tano na cha sita kuwa walimu wa kike
wanajihusisha kimapenzi na wanafunzi hao wa kiume jambo ambalo pia
kisheria haliruhisiwi na ikibainika hatua za kisheria lazima zifuatwe.
Post a Comment
karibu kwa maoni