Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Jonathan Lema amemtaka Mkuu wa Jeshi la
Polisi Simon Sirro kulifundisha jeshi lake kufanya kazi kwa weledi na
kwamba siyo kila amri wanayopewa na viongozi wa mikoa na wilaya inaweza
kuwa afya kwa taifa la Tanzania.
Mhe.
Lema amesema hayo leo baada ya kuzungumzia suala la kamata kamata
inayofanywa kwa amri ya wakuu wa wilaya na mikoa na kusema kwa jinsi
jeshi la polisi linavyotumika siyo kila amri itakyotolewa itakuwa na
maana ndani ya nchi kwani zigine zitalipeleka pabaya taifa la Tanzania.
"Hizi amri ambazo zinatolewa
na kutekelezwa sizo nzuri. Mfano DC siku akisema Mbunge wa Arusha
mjini apigwe risasi basi amri hiyo itatekelezwa nitapigwa. Kwa staili
hii najua wapo watu ambao watakuja nyuma yetu au wengine ambao tupo nao
sasa hivi watashindwa kuvumiliwa haya mateso na udhalilishwaji, ambao
haipiti wiki mbinge wa upinzani anakuwa amekamatwa. Nakemea sana jambo
hili," Lema alifunguka.
Pamoja na hayo Mhe. Lema amempongeza
Rais Mteule wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta kwa kuonyesha demokrasia ya
kweli ya kuruhusu maandamano ya kuupinga ushindi wake huku akitoa na
jeshi la kuwalinda raia katika maandamano hayo.
Post a Comment
karibu kwa maoni