0
Responsive imageMkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amezitaka kamati pamoja na bodi za shule kujiepusha na  kuingiza masuala ya siasa katika utendaji wao.

Gambo amesema hayo wakato wa kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya Arusha  pamoja na walimu wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha,Dakta Wilson  Mahela, amesema Halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari,Charles John,amesema huangalia vigezo vya walimu kwenda kusoma kulingana na taratibu.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,akizungumzia kuhusu bodi za shule amesema zinatakiwa kufanyakazi kwakufuata utaratibu pasipokuingiliwa ili kuongeza ufanisi.

Kuhusu suala la uendeshaji wa vikao vya baraza la madiwani,Gambo,amesema ni vyema kila mtu akaheshimu mipaka ya kazi yake pasipokuingiliana.

Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano katika Halmashauri ya Arusha ilyopo wilaya ya Arumeru.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top