Katibu
Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Dorothy Semu, anatarajia kufanya
ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya Tanzania Bara akiambatana na
viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Ziara
hiyo ya siku nane itaanza tarehe 30 Januari 2018 hadi Februari 6, 2018
kwenye mikoa ya Kahama ambao ni Mkoa Maalum wa Kichama, Kigoma, Katavi,
Shinyanga, Tabora na Kigoma.
Aidha
taarifa ya Chama hicho imebainisha kuwa katibu ataambatana na Ndg.
Wilson Mshumbusi ambaye ni Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa, Ndg.
Janeth Rithe ambaye ni Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa pamoja na
Katibu wa Sera na Utafiti Ndg. Idrisa Kweweta.
Moja
ya majukumu ambayo Dorothy Semu atayafanya ni kukagua uhai wa Chama,
kutoa maelekezo ya ujenzi wa chama, kusikiliza Kero na changamoto za
wanachama na kuzipatia ufumbuzi.
Mbali
na hayo Katibu Mkuu huyo pia atakagua maendeleo ya zoezi la uchaguzi wa
ndani ya chama. Ziara hiyo pia imeelezwa kuwa itawalenga wanachama na
viongozi wa ACT Wazalendo wa maeneo hayo.
Post a Comment
karibu kwa maoni