0

Chama cha mapinduzi  CCM kupitia umoja wa wanawake Tanzania UWT kimefafanya uchaguzi wake wa wenyeviti  na wawakilishi wengine ngazi za wilaya nchi nzima.
Uchaguzi huo ndani ya mkoa wa Manyara umefanyika katika wilaya  sita huku wilaya ya Simanjiro ukisogezwa mbele hadi September 23 kwa sababu ya mabadiliko yaliyofanywa na Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi wa chama hicho Taifa Humphrey Pole pole.
Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni Mwenyekiti UWT wilaya ya Babati mjini na vijijini,wajumbe katika mikutano ya ccm katika ngazi za wilaya na taifa.
kura zilizopigwa kumchagua mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania [UWT] wilaya ya Babati ni 298 kura moja [ 1]iliharibika, hivyo kura halali zilikuwa  297,mgombea Selina Bayo akipata kura 137 huku Naomi Richard aliepata kura  158 akitangazwa kuwa mshindi na kukabidhiwa kiti cha mwenyekiti uwt wilaya ya BABATI.
Nafasi ya mjumbe mwakilishi  uwt wagombea walikuwa wawili,Fatuma hamad  alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 150 huku akimshinda Chiku Juma aliepata  kura 146.,Uwakilishi jumuiya ya vijana CCM Uvccm amepita bila kipingamizi Penina Masanja,Mjumbe mkutano mkuu taifa amechaguliwa Mariamu Kwimba aliepata kura 137 akiwashinda wenzake wawili.
Nafasi nyingine ni mjumbe mkutano mkuu ccm wilaya imeenda kwa Elizabeth Manda  kwa kura 141,mjumbe wa hamlashauri kuu ya CCm ni Lucy Manda kura 204,wajumbe wa baraza walikuwa 11 na walihitajika wajumbe sita ambao ni Naomi Richard kura 154,Elizabeth Manda kura  170,Hadija Juma kura 185,Asha Hassan 218,Lucy Manda kura  220, pamoja na Anna William  aliepata kura 228.
Waliochaguliwa  kushika nafasi hizo wameahidi  kuwatetea wakina mama na kurudisha hadhi ya Chama hicho katika maeneo yao.
Kwa mujibu wa katiba Ya Chama cha Mapinduzi uchaguzi wa jumuiya za chama ngazi ya wilaya  unasimamiwa  katibu tawala wilaya ambapo kwa  Babati  uchaguzi ulisimamiwa na Cade Mshamu ambaye  alitangaza matokeo na kwapongeza wagombea walioshindwa kukubali matokeo hayo huku akikisisitiza kufanya kazi kwa bidii.
Kwa upande wa babati mji aliechaguliwa  kushika nafasi ya mwenyekiti  ni Claudia Haule aliepata kura 89,Mjumbe mkutano mkuu taifa ameshinda Zainabu Zuberi kwa kura 72 huku nafasi ya Baraza wilaya ikienda kwa Neema Ramadhani aliepata kura 97.
Naye Katibu wa UWT mkoa wa Manyara Hainess Munisi akawasihi wanawake wa Ccm babati kuhakikisha hawarudii kufanya makosa kama mwaka 2015 ambapo kata nyingi zilichukuliwa na wapinzani.
Wengine ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika uchaguzi huo na wakapita kwa kishindo.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top