0






Chama cha mapinduzi 
CCM kupitia umoja wa wanawake Tanzania UWT kimefafanya uchaguzi wake wa
wenyeviti  na wawakilishi wengine ngazi
za wilaya nchi nzima.
Uchaguzi huo ndani ya mkoa wa Manyara umefanyika katika
wilaya  sita huku wilaya ya Simanjiro ukisogezwa
mbele hadi September 23 kwa sababu ya mabadiliko yaliyofanywa na Katibu wa
Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi wa chama hicho Taifa Humphrey Pole pole.
Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni Mwenyekiti UWT wilaya ya
Babati mjini na vijijini,wajumbe katika mikutano ya ccm katika ngazi za wilaya
na taifa.
kura zilizopigwa kumchagua mwenyekiti wa Umoja wa wanawake
Tanzania [UWT] wilaya ya Babati ni 298 kura moja [ 1]iliharibika, hivyo kura
halali zilikuwa  297,mgombea Selina Bayo
akipata kura 137 huku Naomi Richard aliepata kura  158 akitangazwa kuwa mshindi na kukabidhiwa
kiti cha mwenyekiti uwt wilaya ya BABATI.






Naye Katibu wa UWT mkoa wa Manyara Hainess Munisi akawasihi
wanawake wa Ccm babati kuhakikisha hawarudii kufanya makosa kama mwaka 2015
ambapo kata nyingi zilichukuliwa na wapinzani.
Wengine ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika
uchaguzi huo na wakapita kwa kishindo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top