0
Katikati ni Alhaj Sheikh Shabani Msii  akiwa ameshikana mkono na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mohammedi Hamisi Kadidi kulia pamoja na sheikh wa wilaya ya Babati.
Mahujaji waTanzania wameanza kuwasili nchini tangu walipoelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa nawatu mbalimbali duniani.
Kwa mwaka huu mkoa wa Manyara mahujaji wawili kutoka wilaya ya Babati walipata nafasi ya kwenda kutimiza nguzo hiyo kuu na muhimu ya dini ya kiislam,ambao ni Alhaji Sheikh Shabani Msii pamoja na Alhaji Sheikh Nuhu Ibrahim Ngaso ambapo wamewataka waislamu na wasio waislamu kutenda yale ya kumpendeza Mungu.
Vijana wa Madrasa wakitumbuiza kwa Kaswida.

Akizungumza na kituo hiki Alhaji Sheikh Nuhu Ngaso amesema kuwa wapo wislamu wengi wangependa kwenda hijja ila wanakosa hamasa kutoka kwa viongozi wao na kuwataka viongozi kusisitiza hio.
Naye sheik mkuu wa mkoa wa Manyara Mohammad Hamisi Kadidi  akawaagiza viongozi wote  wa dini ya Kiislam mkoa wa Manyara kutoa
elimu kuhusu hijj.
Wakina mama nao hawakubaki nyuma walijitokeza kuwalaki Mahujaji.

Mamia ya waislamu mkoani hapa walijitokeza kwa wingi kuwalaki mahujaji hao ambao walifikia katika msikiti wa Bakwata Babati mjini na hatimaye kuwatembelea na kuwasalimu waislamu waliopo Galapo na Mamire.
Alhaji Shabani Msii akisoma dua.
Ibada ya Hijja mwaka huu inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti hadi mwanzoni mwa mwezi Septemba, huku jumla ya mahujaji 977 kutoka Tanzania wameshawasili katika miji ya Madina na Jeddah. Mahujaji hao waliwasili katika viwanja vya ndege vya Madina na Jeddah na kupokelewa na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.
Alhaji Sheikh Nuhu Ibrahim Ngaso akiwasomea dua waislam,Watanzania na nchi yetu katika viwanja vya ofisi kuu ya BAKWATA Manyara.

Tanzania kwa mwaka huu inataraijiwa kupeleka mahujaji wapatao 2,700. Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kupeleka mahujaji wengi mwaka huu inatarajiwa kuwa na mahujaji wapatao 168,000.
Mwaka huu Saudi Arabia ilipokea tarajiwa kupokea mahujaji zaidi ya 2,000,000 kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni.
Waliondoka hapa nchini kuelekea nchini Saudia Arabia Agust 12 mwaka huu na ndege  kampuni ya ya Oman Air na kurudi Tanzania
Septemba 16 na kupokelewa na ndugu jamaa na marafiki waislam na wasio waislam.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top