Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania zifanye tathimini ya maandalizi ya
msimu ujao kwa wakati na zimpatie taarifa mara moja ili kama yapo
matatizo yatatuliwe kwa muda.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo wakati
akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao alichokiitisha
ofisini kwake mjini Dodoma kujadili mwenendo wa zao la korosho na
ununuzi wa pembejeo.
"Lipo tatizo la tathmini ya
maandalizi ya msimu kutofanyika kwa wakati na kusababisha matatizo
kutotatuliwa kwa wakati. Bodi na Wizara zitoe tathimini ya maandalizi ya
msimu ujao kuhusu vyama vya ushirika vilivyojipanga, upatikanaji wa
vifaa kama magunia na nyuzi, maghala, masoko, mizani, minada, malipo na
mfumo wake," alisema.
Aidha Mh Majaliwa amesema tangu serikali
iamue kusimamia mazao makuu matano ya pamba, chai, kahawa, korosho na
tumbaku hajapata muda wa kukaa na kuongea na wadau wote.
"Serikali imeamua
kufuatilia usimamizi wa mashamba; kusimamia upatikanaji wa mbegu, miche
na pembejeo; kufuatilia uvunaji na mfumo wa masoko ya korosho na pia
kufuatilia mfumo wa ushirika katika baadhi ya mazao. Kwa sasa zao la
korosho linalimwa katika wilaya 50 kwenye mikoa 11 ya Dodoma, Iringa,
Lindi, Mbeya, Morogoro na Mtwara. Mingine ni Njombe, Pwani, Ruvuma,
Singida na Tanga. Ameongeza
Ameongeza kwamba "Katika
msimu wa mwaka 2016/2017 zao la korosho lilikuwa ni moja kati ya mazao
ya kibiashara yenye tija na faida nyingi kwa kuliingizia Taifa fedha za
kigeni kiasi cha dola za Marekani milioni 346.6," alisema na kuongeza
kuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 watendaji hawana budi kujipanga
vizuri ili zao la hilo liendelee kuliingizia Taifa dola nyingi zaidi kwa
kuwa Serikali imetoa viatilifu bure.
"Ninasisitiza eneo hili kwa
sababu tumebaini kuwa korosho inachangia zaidi ya asilimia 50 ya mapato
kwenye Halmashauri zinazolima kwa wingi zao hilo. Kwa kuwa zao hili ni
la kimkakati, naitaka Wizara inipatie taarifa sahihi na kwa wakati," alisisitiza.
Post a Comment
karibu kwa maoni