0
Kesho September 7, 2017 Rais John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya
uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na Kamati maalum
mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Job Ndugai.

Taarifa hiyo itakabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Ikulu Jijini Dar
es Salaam katika hafla itakayorushwa moja kwa moja na vituo vya redio
na televisheni kuanzia saa 4:00 Asubuhi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top