Mfanyabiashara
Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu
kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya
maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.
Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.
Kutokana na hilo wamemuondoa Manji kwenye nafasi hiyo kutokana na kukosa sifa za kuendelea kuwa kiongozi.
Itakumbukwa kuwa Manji alishinda Udiwani katika Kata ya Mbagala Kuu katika Uchaguzi Mkuu wa 2017 lakini amevuliwa kutokana na kushindwa kufanya majukumu yake ya uwakilishi wa wananchi kwa miaka miwili mfululizo.
Post a Comment
karibu kwa maoni