Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewakumbuka waumini wa dini ya Kiislam na kuwatakia sikuu njema ya Eid.
Katika ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ametoa ujumbe huo kuwatakia Eid njema, huku akihimiza kudumisha amani, upendo na mshikamano.
Waumini wa dini ya Kiislam nchini leo wanaungana na Waislam wenzao wote duniani, kusherehekea sikuku ya Eid ambayo huadhimishwa kila mwaka, mara baada ya ibada ya Hija kukamilika, na mara nyingi husherehekiwa kwa kuchinja wanyama waliohalalishwa kwa binadamu.
Post a Comment
karibu kwa maoni