Wanaume nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu kusimamia
afya ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vinavyotokana matatizo ya uzazi na
utapiamlo.
Hayo yameelezwa na mtaalamu wa afya na lishe kutoka shirika
la World Vision Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara Joan Msuya wakati wa wakihitimisha
mafunzo ya wiki tatu kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii Tarafa ya Gorowa wilayani
hapa.
Mtaalamu huyo amesema matarajio ya shirika hilo kupitia
mafunzo waliyoyatoa,wanaamini jamii itahamasishwa pamoja na kutoa elimu sahihi
za afya na Lishe katika ngazi ya kaya na katika vituo vya kutolea huduma.
Joan ameeleza kuwa wanategemea ushiriki mkubwa kwa wanaume
katika masuala ya afya na Lishe ya mama na mtoto na hatimaye kupunguza vifo vya
watoto pamoja na wanawake vitokanavyo na uzazi na matatizo ya utapiamlo kwa
watoto tarafa ya Gorowa.
Akizungumza baada ya kuwatunuku vyeti walipata mafunzo
hayo,mkurugezi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Idd Malinga
amewataka walipata mafunzo hayo wakawe chachu ya kuibadilisha jamii na
kupunguza matatizo ya Uzazi na utapiamlo kwa watoto.
Shririka la Worl Vision Tanzania [WVT] limekuwa likiendesha
program mbalimbali za maendeleo ya jamii katika maeneo tofauti tofauti kupitia
miradi yake 45 iliyopo Tanzania.
Miongoni mwa maeneo ya mradi ni pamoja na Gorowa ADP ambayo
ipo ndani ya Halmashauri ya Babati mkoani Manyara na imekuwa ikiwawanufaisha wanajamii wa
Gorowa kwa kuwasaidia kujikwamua
kiuchumi katika kuwapatia wana vikundi mikopo,kujenga shule kupitia mradi wa
watoto tusome,kutengeneza kambi za watoto za kujifunzia,kununua vitabu na
kuvisambaza mashuleni na kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu
katika mahitaji muhimu ya watoto ikiwa ni pamoja na elimu.
Aidha shirika hilo kwa kujali umuhimu wa Mazingira limewahimiza
wakazi wa kata ya Riroda kutunza misitu kwa kuwapatia miche ya miti 35,000 ili kuboresha
hali ya hewa.
Shirika llimejenga mifereji ya kumwagilia katika vijiji vya
Sangara na Ayasanda iliyogaharimu ziadi ya Tshs.152,000,000.
Kwa upande mwingine shirika limejenga chuo cha mafunzo ya
Ufundi [VETA] katika kijiji cha Ayasanda ambapo hivi karibuni kitakabidhiwa kwa
serikali ili kuwezesha vijana kupata mafunzo mbalimbali ya Ufundi na hatimaye
waweze kujiajiri wenyewe.
Vile vile shirika liko mstari wa mbele katika kuboresha Afya
na lishe ya Jamii hususani kwa Mama na mtoto,na
Katika kuhakikisha afya na lishe ya Mama na Mtoto inaborshwa shirika
limeendelea kutoa mafunzo jumuishi ya afya na lishe kwa watoa huduma za afya katika
ngazi za jamii na vituo vyote vya afya katika kata ya Gorowa .
‘Lengo la kuwapatia mafunzo WAJA ni ili wapate ujuzi na elimu ya lishe kuweza
kuleta mabadiliko chanya ya afya na lishe katika jamii’.alisema Joan
Katika mafunzo hayo jumla ya WAJA thelethini na tano [35]
pamoja na wasimamizi wao saba [7] kwenye vituo vya kutolea huduma na wasimamizi
wawili kutoka CHTMT wamepata mafunzo hayo.
Washiriki hao wakizungumzia mafunzo hayo waliyopatiwa na
wawezeshaji kutoka wizara ya afya,ustawi wa jamii,jinsia wazee na watoto
wamesema kuwa yatawawezesha kuisaidia jamii iliyokuwa haina uelewa wa lishe kwa
Mama na mtoto.
‘Jamii zetu hazijui ni muda gani motto anapaswa kunyonyeshwa
baada ya kuzaliwa,hivyo kwa mafunzo haya tuliyoyapata tutayapeleka kwa kina
mama ili wawanyoshe watoto wao kwa muda wa siku 1000’. Walisema WAJA.
Baada ya mafunzo hayo walipatiwa mizani saba za kisasa zenye
thamani ya shilingi milioni 10,380,000 zenye uwezo wa kupima uzito wa Mama na motto
kwa wakati mmoja hatua inayorahisisha utendaji wa kazi katika vituo vya afya.
Post a Comment
karibu kwa maoni