0
Ni stori ya kweli iliyomtokea binti mmoja wa kabila la Iraq [Mmbulu] amabye alipata mimba kabla ya kuolewa ndipo familia ikamtenga ikiaminika kuwa kupata mimba wakati bado hujaolewa ni laana,wazee waliamua kumtenga binti huyo ajulikanaye kwa jina la Imbori kisha kumtelekeza pori lenye wanyama wakali ili amalizwe kabisa.
Lakini kijana aliepatia mimba ambaye hakutajwa na binti wala hakujitokeza anayejulikana kwa jina la Mayo alijua kilichotokea akaamua kumfuata binti huyo na kumwokoa hatimaye kwenda naye mpaka eneo lililojulkana kama Imboru enzi hizo kabla ya sasa kuitwa Mbulu ambayo ni wilaya iliyopo mkoani Manyara. Mbulu ndio sehemu inayotajwa kuwa na wasichana warembo wa kuvutia.Stori hii Inakadiriwa kuwa ni zaidi ya miaka 500 iliyopita.
Kitila ameumiza sana kichwa kuutunga wimbo huu ulioturudisha mpaka miaka ya sasa ikisisitiza Msamaha na kuheshimu wazazi huku tukiishi kwa kumtegemea Mungu
Wimbo wenyewe huu hapa tuusikilize ameimba kwa hisia sana msanii anayefanya vizuri kwenye muziki huu wa kizazi kipya Tanzania BOY KITILA.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top