0
Wanachama wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mbeya mjini, wametishia kutotoa ushirikiano kwa Mwenyekiti mpya wa UVCCM, Stephano Halinga, aliyeshinda uchaguzi mwishoni mwa wiki kwa madai kuwa mchakato wa kumpata Mwenyekiti huyo ulikuwa na shinikizo.

Wakizungumza mara baada ya uchaguzi huo, baadhi ya wanachama hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao walizielekeza lawama zao kwa Katibu wa UVCCM, Gerald Kinawiro na Katibu wa CCM Mbeya Mjini, Gerald Mwadallu kuwa walihusika na uteuzi wa Mwenyekiti mpya.

Akijibu tuhuma hizo Katibu wa UVCCM, Mbeya Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa uchaguzi, Gerald Kinawiro, amedai kuwa, mchakato wa kuwapata wagombea unafanywa kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama, hivyo hujuma hizo hazina ukweli wowote na kama kuna mwanachama yeyote mwenye malalamiko afike kwenye ofisi za chama.

Katika kiny’ang’anyiro cha kumpata Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya mjini Stephano Halinga alipata kura 178, Farida Ngoyi kura 61 na Omari Omari kura 60.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top