Uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti mpya wa ccm Babati vijijini umefanyika baada ya kuwa umeaahirishwa siku ya ijumaa kutokana na sababu mbalimbali huku mgombea alieshindwa akikiri kuwa alitoa rushwa.
Katika uchaguzi huo wagombea walikuwa wawili baada ya mmoja
kujitoa na baada ya kura zote kuhesabiwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Martha
Umbura akatangaza matokeo ambapo
Gabriel alipata kura Lusian
378,na Abdilahi Sogora akatangazwa kuwa
mwenyekiti kwa kupata kura 399.
Aliyechaguliwa sasa alikuwa akitetea nafasi yake hivyo ataongoza tena
kwa miaka mingine mitano na kufanya muda aliongoza madarakani kufikia miaka 20.
Katibu wa ccm wilaya ya Babati vijiijini anaeleza kuwa
hakuna mgombea aliekamatwa na rushwa na kwamba chama hicho kinachoongozwa na
Mwenyekiti Rais John Pombe Magufuli kinapiga vita vitendo vya Rushwa.
Aidha katibu amesema kuwa chama kwa sasa kimejipanga
kubadilisha mfumo katika kutoa majina ya wagombea katika chaguzi zinazokuja
kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka uchaguzi mkuu ili kuepuka vitendo vyovyote vya ushawishi
kwa wapiga kura.
Uchaguzi wa mwaka huu tumeshuhudia viongozi wanaoshindwa
kulalamika na kusema rushwa imetumika katika kushawishi wajumbe.
Katibu wa Ccm Babati vijijini Edna Edmund Khera amekiri kuwa
Rushwa Na ukanda ni mambo ambayo yamegubika kwa kiasi kikubwa katika uchaguzi
wa mwaka huu na kuwataka wanachama wanapohisi vitendo vya rushwa watoe taarifa
mapema au wapekeke ushahidi.
Mwenyekiti aliechaguliwa Abdilahi Sogora akawashukuru
zuyngumza haya huku akiwashukuru wanachama kwa kumchagua tena.
Uchaguzi wa chama cha Mapinduzi ngazi ya wilaya umekamilika
na kwa sasa unaofuata ni chaguzi katika ngazi ya mkoa mwezi novemba mwaka huu.
Post a Comment
karibu kwa maoni