0

Meneja wa Bank ya CRDB Babati Ronald Paul akizungumza na wateja wa bank hiyo katika kilele cha wiki ya mteja.
Kutokana na kuwa Asilimia kubwa ya ya Wakazi wa Mkoa wa Manyara ni wakulima na Wafugaji na wengi wao kutotumia huduma zozote za Benki,Benki ya CRDB tawi la Babati Mkoani Manyara wametakiwa kuboresha huduma zao ili hata wakulima na wafugaji wapate fursa mbali mbali zinazotolewa na benki.
Meneja wa CRDB tawi la Magugu Babati Bwana Bruno kulia akiwa na mtoa elimu kwa wateja CRDB Bwana Amani  Babati mjini.
Afisa elimu mkuu wa mkoa wa Manyara Arnold Msuya [kushoto]akiwa ameongozana na meneja wa CRDB Babati Ronald Paul [kulia]katika kilele cha wiki ya mteja iliyofanyika katika viwanja vya bank hiyo Babati mjini.


Akizugumza katika kilele cha  wiki ya Huduma kwa Wateja
yaliyofanyika Wilayani Babati juzi Kaimu Rass Mkoa huo Anold Msuya alisema bado kuna idadi kubwa ya wananchi, wakulima wanaokaa na fedha zao majumbani kwakidhani kupeleka fedha benki ni usumbufu.

Alisema asilimia kubwa ya watu hao hawaoni umuhimu wa kuweka fedha benki kwa kuogopa kukwatwa fedha zao,na kuogopa usumbufu wa kila mara wa kufuata fedha Benki.

“Mkulina anaona kuna umuhimu gani wa kupeleka fedha Benki ikakatwe wakati naweza kuiweka ndani, bila kujua anakosa fursa nyingi kiama vile ya mikopo ya pembejeo za kilimo,ni vizuri kama Benki itafanya kazi ya Kutoa Elimu kwa wakulima,wafugaji,kwamba kutumia huo ukulima anaweza hata kupata mkopo na
akajiendeleza’’alisema Msuya.

Aliwataka Benki kuangalia namna ya Kupunguza Riba ya mikopo hasa kwa Wakulima kwani wengi wa Wafanyabiashara sikuhizi wamekuwa waoga kuchukua mikopo kutokana na riba kubwa wanayotozwa.

Aidha aliwapongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha Huduma mpya ya Premium Bank huduma  ambayo inawawezesha wafanyanbiashara wakubwa kutoa fedha zaidi ya milioni 10  kwa maramoja kwa kutumia ATM kadi tofauti na awali ambapo mteje anaweza kutuoa kisi cha shilingi million moja tu kwa siku.

Kwa Upande wake Meneja wa CRDB  Mkoa huo Ronald Paul alisema licha ya wao kujitahidi kutoa mafunzo ya Biashara na Mikopo kwa  wajasiriamali lakini changamoto imekuwa kwa wajassiriamali hao kutorejesha mikopo hiyo kwa wakati,na wakulima wengi kutoweka fedha Benki hata wakiuza mazao yao.

‘’Tuna Bilioni 15.7 katika tawi hili ambazo kabla hatujafungua CRDB
zilikuwa zinawekwa kwenye mito,kupitia fedha hizo tutaendelea kuinua uchumi wa kila mtu katika Mkoa huu kwa sasa tumepiga hatua, hospitali zote  za mkoa huu malipo yake yanafanywa kwa kadi na tumeshakopesha kiasi cha shilingi billion 12.3 kwa watumishi wa Serikai na wafanyabiashara’’ alisema Paul.

Alishauri mkoa uache kutegemea fursa moja tu ya Kilimo na badala yake mkoa ujikite katika Kutengeneza viwanda ,na utalii kutokana na na Mkoa huu kuwa na fursa nyingi ambazo bado  hazichangamkiwi na kwamba wao kama benki wapo tayari kusaidiana katika Kuibua fursa nyinginezo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top