#Anaandika Suleiman Ussi kutoka Zanzibar.
Ligi kuu soka
ya Zanzibar imeendelea tena leo kwa kupigwa michezo miwili majira ya saa8 za
mchana CHARAWE wamekubali kipigo cha mara ya pili cha mabao 4-0 dhidi ya timu
ya KIPANGA charawe wanaonekana bado kuwa
wageni wa ligi kuu ya soka ya Zanzibar.
Mchezo wa pili
umepigwa majira ya saa10 za jioni kati ya timu ya KILIMANI CITY wakioneshana
kazi dhidi ya timu ya KMKM na katika mchezo huo timu ya kmkm wakaibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya
timu ya kilimani city .
Ligi kuu ya zanzibar itaendelea tena siku ya kesho
kwa kupigwa mchezo mmoja tu majira ya saa10 za jioni BLACK SAILOR vs JAN’GOMBE
BOYS ..
ZFA wilaya ya
mjini imeanzisha darasa maalumu la kuwafunza uwamuzi vijana wadaogo wenye umri
kuanzia miaka 13 akizungumza na kipindi hiki mkufunzi huyo ambae pia ni katibu
wa waamuzi Ramadhani ibada kibo amesema vijana hao wadaogo wanapopewa mechi
kubwa kuchezesha wanajifariji sana na kusema vijana hao pia wameshachezesha
mashindano ya Rulingi stone huku Tanzania bara huku akiwata vijana wengine
pamoja na wanawake kujifunza suala zima la uwamuzi ,,
Baada ya siku
ya jana kumalizika kwa zoezi zima la upitishaji kwa madaraja ya vijana wilaya ya mjini timu mbali mbali zimeanza
maandalizi ya mazoezi ya ligi za Jivanili, Junio ,na central kipindi hiki
kilifanikiwa kuzungumza na kocha wa Jivanili wa timu ya River side Hafidhi amesema timu yake msimu huu
wamejianda kwa kuchukua ubingwa pia ametoa changamoto mbali mbali
zinazowakabili katika ligi hizo za vijana
ni ukata wa wazamini pamoja na zawadi.
Baada ya siku
ya jana timu ya kwerekwe city inayoshiriki ligi daraja la pili taifa kutoka
suluhu ya kufungana bao 2-2 didi ya timu ya Zantex inaendelea na mazoezi makali ya kujianda na
mchezo wao ujao dhidi ya timu ya Bweleo katibu mkuu wa timu hiyo ya kwerekwe
city mussa mzirai amesema mapungufu yaliojitokeza jana watahakikisha
wanayafanyia kazi ili timu yao ifanikiwe kushinda katika michezo ijayoo..
Post a Comment
karibu kwa maoni