Mkuu wa mkoa wa Mara Dr. Charles Mlingwa ameipongeza
Halmashauri ya mji wa Bunda kwa kuonyesha utayari wa kujenga kiwanda cha nyama
ndani ya halmashauri yao ambapo amesema ni moja ya hatua kubwa ambayo itasaidia
kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Dr.Mlingwa ametoa pongezi hizo leo wakati akikagua
eneo litakalojengwa machinjio ya kisasa na kiwanda cha kusindika nyama katika kata ya Bunda stoo Halmashauri ya mji
wa Bunda.
Dr.Mlingwa amesema anataka kuona kiwanda cha nyama
kinaanzishwa ndani ya mkoa wa Mara hivyo amesema kwa kuwa Halmashauri ya mji wa
Bunda wameonyesha nia ya kuanzisha kiwanda hicho ameahidi kutoa ushirikiano
mkubwa kakamilisha mradi huo.
Hata hivyo Dr.Mlingwa amesema anafahamu kuwa wapo
wananchi watakao hitaji fidia kupisha mradi huo hivyo amewaomba waondoe shaka
na kwamba kila mtu atapata haki yake kwa wakati bila shida yeyote na kuwataka
kuanza maandalizi ya kupishisha eneo hilo.
Post a Comment
karibu kwa maoni