0
Jioni ya leo april 13.2018 gari [LORI]ya  Kampuni moja ya kuchimba visima ya mkoani Arusha imeteketea kwa moto.

 Ilikuwa ikitokea Arusha kuelekea Dodoma,ilipofika Babati eneo la Changarawe likachemka na kuteketea kwa moto.
 Licha ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji  Manyara kufika eneo la tukio ilikuta tayari moto huo umeshateketeza nusu ya gari hilo lililokuwa limebeba Mashine ya kuchimbia Visima ambapo dereva na msaidizi wake waliwahi kuruka kwenye gari hilo lililoanza kuwaka upande wa dereva na kufanikiwa kuokoa baadhi ya vifaa vilivyokuwa vimepakiwa na gari hiyo..

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top