0
Miaka ya 2006-2007 Boti ya kisasa kwa ajili ya kufanya ukaguzi ndani ya ziwa Burunge kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara ilinunuliwa kwa gharama ambazo sijazipata ila naamini ni pesa nyingi zilitumika.
Boti hizo zilitolewa na serikali kwa ajili ya kufanya doria katika Maziwa yote yanayopatikana ndani ya mkoa wa Manyara ila cha kusikitisha mpaka sasa hakuna boti inayopatikana katika maziwa ya Manyara zaidi ya Mitumbwi inayotumiwa na wavuvi.
Kinachoonekana hapo ni kwamba baada ya boti hizo kuharibika hazikufanyiwa marekebisho yeyote na badala yake zikaachwa zikawa ndio makazi ya Mbu na vyura.
Hii ni moja kati ya Boti inayojukana kama MV.BABATI No 2 niliyoikuta eneo ambalo ilikuwa Ofisi za TEMESA ambayo kwa  sasa ni ofisi ya UJENZI [TARURA]  wilayani Babati.
Kwa hiyo tangu kuharibika kwake hadi leo haijatengenezwa hivyo hakuna boti ya doria ili kuangalia hali ya usalama na kuzuia wavuvi haramu katika maziwa yetu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top