|
Katika zoezi
hilo,jumla ya vituo 51 katika kijiji cha Sebasi kilichopo kata ya Gendabi
vinavyotiririsha maji kwenda katika kata ya Dawar vilikatwa na kusababisha
mgogoro ulioingiliwa kati na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo
kutokana na wananchi wa kata ya Dawar kukesha nje kwa takribani mwezi mmoja
wakipinga zoezi hilo.
Akizungumza
na wakazi wa kata ya Dawar na Gendabi Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ Bi.Sarah Msafiri alisema kuwa ili
kuepuka mgogoro huo kutoendelea ni lazima kuwepo na utaratibu sahihi wa maji kwa watumiaji ili
kuepuka lawama wanazotupiana kati yao ambapo kila kata imekuwa ikiwatuhumu wenzao wanatumia maji vibaya.
Wakazi wa
kata ya Gendabi wameelezwa kuwa wao ni walimaji wa mbogamoga ambazo zinahitaji
maji mengi kwa ajili ya kumwagiliwa huku wakazi wa Dawar wakielezwa kuwa na
mifungo mingi inayohitaji maji mengi
kwenye unyweshwaji
‘’Ninachotaka kuwaambia ni kitu kimoja tu ndugu zangu ili mgogoro huu uishe kwanza ni lazima mjue hiki ni kipindi cha kiangazi maji huwa yanapungua siyo mengi kama kipindi cha masika,mnachotakiwa kukifanaya kwa sasa kwa kuwa gendabi mnalima mbogamboga mnamwagilia maji punguzeni ulimaji huo limeni kiasi kulingana na upatikanaji wa maji’’alisema Bi.Sarah
Wakazi wa vijiji vya Gendabi na Dawari hutumia maji yananatokana na
chanzo kilichokuwa katika kjiji
cha Gendabi kinachotoka mlima Hanang.
Stephen
Sulley ni diwani wa gendabi alieleza kuwa vijiji hivyo vinachangamoto ya
kukosa mahusiano bora kati yao huku pia wanasiasa wakitumia tatizo la ukosefu wa maji kwa kuwarubuni wananchi kuwekeana chuki baina yao.
‘’Mkuu wa wilaya mimi naona kata hizi mbili ni kama tunaoneshana ubabe tu kwa sababu hapa siyo kwamba hakuna maji, maji yapo ila utaratibu unaotumika ndio mbovu sisi hawa jirani zetu Dawar tumewapa chanzo cha maji wakitumie lakini bado wanatuona wabaya wanakuja kwetu na kukata mita zote za wanakijiji sisi makosa yetu ni yapi?’’alisema Diwani Sulley.
Mkuu wa
wilaya pia amevunja jumuiya ya maji iliyokuwepo kutokana na jumuiya hiyo
kushindwa kufanya kazi yake ambayo ni
kusimamia mradi na kuripoti sehemu husika huku akitoa agizo kwa kata zote mbili
kuunda jumuiya nyingine ndani ya wiki moja.
Post a Comment
karibu kwa maoni