0

 

Leo ni siku ya marudio ya uchaguzi na pia ni siku sawa na aliyozaliwa Rais Uhuru Kenyatta mwaka 1961.

Baadhi ya idara za serikali zimechukua fursa hii kumtumia salamu za heri. Mvua GithuMvua Githu

Wapiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Kimbo katika eneo la Githurai 45, Kiambu wamevumilia mvua na baridi kali kwenye foleni kusubiri fursa ya kupiga kura.

Mvua imenyesha katika maeneo mengi Kenya usiku wa kuamkia leo.


Katika baadhi ya maeneo Kisumu, ngome ya Raila Odinga, baadhi ya wafanyakazi wa tume ya uchaguzi waliofaa kuendesha uchaguzi wa leo hawajafika vituoni bado.

Msimamizi wa uchaguzi kituo cha shule ya sekondari ya Lions High ameambia BBC kwamba kati ya wafanyakazi 399 eneo hilo, ni watatu pekee waliojitokeza.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top