Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea nyumba za askari polisi zinazojengwa
mkoani Arusha baada ya kuteketea kwa moto na kuwapongeza
wananchi kwa kujitolea kuwachangia fedha ili wapate makazi mapya.
Hivi karibuni jeshi la
polisi jijini Arusha lilipata pigo baada ya Familia 13 zenye watu 44 kuunguliwa
nyumba zao katika mtaa wa Sekei.
Akizungumzia hali ya usalama nchini Mwigulu amesema kila
anaetenda maovu lazima akamatwe na kwamba hakuna muhalifu popote pale
atakaebaki salama.
Waziri Nchemba amefika jijini Arusha akitokea mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro kwenye ufunguzi wa maazimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama Bara
barani kitaifa yaliyofunguliwa na makamu
wa rais Mama Samia Suluhu Hassan.
Post a Comment
karibu kwa maoni