Imeeleza kuwa wananchi wengi
wanakosa haki zao kutokana na uelewa mdogo kuhusu sheria jambo linalosababisha
ukatili, unyanyasaji kwa wanawake katika migogoro mingi ya familia .
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Kituo cha usaidizi wa kisheria Wilayani Mbulu (MPAC) Ezekiel Assecheck wakati akizungumza na Gazeti hili ofisini kwake ambapo alisema kwamba wanawake wengi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huku wakiwa hawajui pa kwenda kupata haki yao.
Alisema kuwa Kituo hicho juni 2017 kilipokea kesi 15 zilizopata suluhisho kati ya hizo 13 zilihusu wanawake waliokuwa wakikabiliwa namatatizo ya migogoro ya ardhi lakini pia na migogoro ya kifamilia.
“Dhamira ya Kituo chetu ni
kuiwezesha jamii kufahamu sheria na wajibu wa kutetea haki wakati wote kwa
kutoa elimu ya sheria ili wananchi watumie katika kuleta maendeleo” Alisema
Assecheck.
Aidha kituo hicho kimeweka mkakati
wa kufundisha sheria katika mikutano ya hadhara inayohusu masuala ya
ndoa, ukatili na migogoro ya ardhi kusuluhisha kesi zinazojitokeza za mtu mmoja
mmoja na vikundi.
Hata hivyo kituo hicho kimeweza
kuwafikia wananchi zaidi ya 800 kwa mwezi Agasti na kuwapatia elimu na msaada
wa kisheria .
Post a Comment
karibu kwa maoni