Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Bi. Janeth Masaburi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Mhe.
Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1)(e) ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kuteua
wabunge 10 watakaokuwa miongoni mwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Bi. Janeth Masaburi ataapishwa kulingana na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
Post a Comment
karibu kwa maoni