0
NA GHAROS RIWA -BUNDA
Siku chache kupita serikali ya Tanzania kufanya mazingumzo na mkurugenzi wa barick na kukubaliana kulipa shilingi bilioni 700 na baadae kampuni ya uchimbaji madini ya acacia kutangaza kuwa hawana fedha ya kulipa, hatimae Mheshimiwa Pastory Ncheye diwani wa kata ya kabalimu katika halmashauri ya mji wa Bunda Mkoani Mara amemkosoa mbunge na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo zito kabwe kwa kumuelezea kuwa haelewi  anachokizungumza.

Amesema hayo leo wakati wa maojino na  redio mazingira fm cha mjini hapo ambapo ameeleza kuwa anawezekana haelewi anachokizungumzo kwasababu yeye ni mbunge anaetokana na chama kingine ambacho sio tawala hivyo hajajua vizuri kwa sasa chama cha mapinduzi kinafanyaje kazi.

Amesema kwamba yeye anavyoamini[pastory] serikali ya awamu ya tano inayoendeshwa na mheshimiwa John Pombe Magufuli haina vitu vya ‘kujaribu’ .

Hivi karibuni zito kabwe amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa serikali inachezewa na makampuni ya kimataifa yanayochimba na kuuza madini, ambpo barik imewaihi kutoa ahadi katika nchi mbalimbali kama chile,equdoe na bolivya na hivyo watu wanajazwa upepo na kuonya kwamba ni mapema sana Tanzania kujitangazia ushindi katika kupata bilioni 700 .
Amesema kwamba ikitokea kwamba Barick wakapuuza mazungumzo yaliyofanyika na tayari walishawekeana mikataba basi mikataba hiyo itafanya kazi.

maana ya kufanya mikataba lengo lake lilikuwa ni ushuhuda kwamba walichokubaliana pande zote mbili zinaridhia’ alisema Ncheye.

Ncheye amesema kama alivyomsikia mkurugenzi wa barik haamini kama huko mbele kutakupo na ‘ukigeugeu’.


Amesema kuwa matatizo haya ya madini yanatokana na baadhi ya watanzania kukosa uzalendo lakini katika uongozi wa awamu hii ya tano tatizo hilo halipo.

Ncheye ameelezea kwamba viongozi waliopo kuanzia Rais mwenyewe na mawaziri wake na wasaidizi wao hakuna mwenye mzaha, hivyo sheria zipo na ndio maana mkurugenzi wa barik amekubali maitaji ya sheria iliyo ya madini.

Amesema kuwa amefatilia vizuri maelezo ya waziri wa sheria na katiba prof Palamagamba kabudi na amebaini kuwa katika mgawanyo wake serikali ya Tanzania inachukuwa kiwango kikubwa zaidi.


Hata hivyo katika ufafanuzi wake mheshimiwa Ncheye amewataka wananchi kuonyesha uvumilivu na kuunga mkono juudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika vita hii ya kiuchumi badala ya kupinga kila kitu. 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top