Mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zari mchana wa leo
Jumamosi alisimamisha shughuli katika maduka yaliyopo Mlimani City
alipokwenda kuzindua duka jipya la samani, Danube.
Wakazi
wa jiji la Dar es Salaam waliofika kufanya manunuzi katika maduka hayo
walijazana nje ya duka jipya la Danube wakitaka kumuona Zari huku
wakiimba wifi... wifi.
Purukushani zilitawala nje ya
duka hilo wakati kila mmoja akijaribu kumsukuma mwenzake ili aweze
kumuona Zari aliyekuwa ameketi katika makochi akizungumza na
wafanyakazi.
Watu walivutiwa kumuona mwanamke huyo
kutokana na hivi karibuni kupamba vichwa vya habari baada ya Diamond
kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.
Ujio wa
Zari nchini amekuwa na mvuto kwa kuwa mashabiki wamekuwa wakilinganisha
matukio katika maisha ya Diamond, Zari na Hamisa.
Siku
moja kabla ya Zari kutoa tangazo kuwa angeshiriki uzinduzi wa duka jipya
la Danube, mwanamitindo Hamisa aliweka tangazo la duka hilo ambalo
liliwahi kufanywa na Diamond na Zari mapema mwaka huu.
Katika
tangazo hilo Zari alisikika akimpiga kijembe mwanamke aliyeacha hereni
nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar es Salaam akimtaka aende
akachue.
Katika posti yake kwenye mtandao wa Instagram,
Hamisa aliandika: “It’s about time nifuate hereni zangu, I hope they
are still there.” Akimaanisha umefika wakati nifuate hereni zangu,
nadhani zitakuwepo.
Post a Comment
karibu kwa maoni