Hizi ni taka taka zilizosambaa katika kizimba kilichopo pembezoni mwa kiwanja cha Kwaraa mjini Babati. |
Wakazi wa mji wa Babati wameiomba Halmashauri kuziondoa
mapema taka zinazokusanywa katika vizimba ili kuepuka kuzagaa ovyo kutokana na
upepo.
Wafanyabiashara wanaozunguka eneo la kizimba cha Kwaraa na soko la Darajani kinachokusanya
taka kwa muda kabla ya kupelekwa dampo kuu katika kijiji cha Gaduet kata ya
Sigino wamesema licha ya kuwaathiri lakini pia linawafukuza wateja wao kutokana
na harufu mbaya inayotekea katika taka hizo ambazo zimekuwa zikikaa kwa muda
mrefu bila kuondolewa.
Muonekano wa kizimba cha taka Kwaraa,taka hizo zinadaiwa kuwepo hapo zaidi ya wiki sasa. |
Akizungumzia hilo katika kikao cha baraza la madiwani
kilichoketi jumatatu ya wiki hii katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Babati
wakati mwenyekiti wa wa Halmashauri Mohamedi Kibiki akifungua baraza hilo
ambalo ni la mwisho katika mwaka huu wa 2017 aliitaka idara husika kusimamia
hilo ilio kuuweka mji katika hali ya usafi.
Mkuu wa idara ya usafi na Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Halmashauri ya mji
wa Babati Faustin Masunga amekiri kuwepo kwa taka hizo kwa muda mrefu huku
akisema kinachosababisha ni upungufu wa Madereva akisema kuwa kwa sasa wanasubiri vibali vipya
vya ajira ili kutatua changamoto hiyo.
Masunga ameawataka wakazi wa mji wa Babati kuchangia huduma
ya kuzoa taka na kutupa taka katika maeneo husika ili kuepuka kuzagaa ovyo kwa
taka taka.
Aidha masunga ameeleza kuwa Halmashauri ina Magari matatu
kwa ajili ya kuzikusanya taka na kuzipeleka Dampo kuu ila zoezi la uhakiki
lilisababisha kuwakosa madereva wa magari hayo,kwa sasa wanasubiri vibali vya
ajira vitoke.
Katika kuhakikisha mji wa Babati unakuwa katika hali ya
usafi hivi karibuni Halmashauri ya mji
ilinunua gari la kisasa lenye thamani ya shilingi milioni 200.
Post a Comment
karibu kwa maoni