0

SERIKALI imeomba wawekezaji wa ndani kuwekeza miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Katibu Mkuu wa Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho ametoa rai hiyo jana Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Mwaka katika Tehama.
Dk Chamuriho alisema Serikali imefanya kazi kubwa katika awamu ya kwanza na ya pili kuwekeza kwenye miundombinu ya Tehama ambapo katika awamu hizo, mkongo wa taifa wa mawasiliano umewezesha makao makuu ya mikoa na baadhi ya wilaya nchini kuunganishwa katika mawasiliano.
Alisema baadhi ya kampuni zimeonesha nia ya kuwekeza katika miundombinu ya Tehama na kwamba mpaka sasa inaonesha hakuna kiwanda ambacho kitafanya kazi vizuri bila kutumia Tehama ipasavyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tehama Tanzania, Maharage Chande waandaaji wa kongamano hilo alisema Tehama ni chachu ya kuongeza kasi ya Tanzania ya viwanda. Chande alisema sekta ya Tehama inabadilika mara kwa mara.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top