GHAROS RIWA & THOMAS MASALU-
BUNDA
Jumla ya wazee 235 katika kata ya neruma wilayani
Bunda Mkoani Mara wamepatiwa
vitambulisho vya msamaha wa matibabu lengo ikiwa ni kuhakikisha wazee
wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu maisha yao
ya kila siku.
Akisoma taarifa ya utoaji wa huduma za afya na stawi
wa jamii Kwa mgeni Rasmi Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya bunda Liberatus
Kazana katika maadhimisho ya siku ya wazee Duniani yaliyofanyika Katika kijiji
cha Neruma kata ya neruma Oktoba 20 amesema Halmashauri ya wilaya ya Bunda
inajumla ya wazee 9,994 waliona miaka 60 na kuendelea.
Kazana Amesema kunachangamoto mbalimbali katika
uendeshaji wa huduma za afya na hasa katika kuwahudumia wazee huku gharama za
uendeshaji wa huduma za msamaha zimekuwa kubwa katika vituo vya kutolea huduma
za afya hiyo ikitokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji msamaha kama vile
akina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano,walemavu na wazee.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni Katibu
Tawala wa wilaya ya Bunda Masalu Kisasira amesema wao kama serikali wanatambua
changamoto hizo hivyo ameahidi kuzifanyia kazi huku akiwasihi wazee kuwa kioo
kizuri kwa watoto wao kwa kuwaonya na kuwashauri ili kuwawezesha watoto wao
kuwa na misingi bora ya maisha.
Post a Comment
karibu kwa maoni