|
Hapa ni katika kijiji cha Dabil kata ya Dabil wilaya ya Babati mkoa wa
Manyara ambao wanakijiji wake bado wanatumia maji yanayotirrika katika
miferiji ambayo kimsingi sio safi na salama. | | |
Lakini Wapo waliozaliwa katika kijiji hiki miaka ya tisini mpaka sasa wanasema hawajwahi kutumia maji yanayotoka kwenye bomba lakini Mungu anawasaidia na hawajawahi kuugua kutokana na matumizi ya maji hayo.
|
Mtandao wa WALTER BLOG katika eneo yanapopatikana maji. |
WALTER HABARI ilifika katika kijiji hicho kil;icho chini ya milima na kushuhudia baadhi ya wanakijiji wakiteka maji kutoka kwenye mfereji unatoa maji katika chem chem ndogo inayotoa maji kidogo na kuwasaidia wakazi hao katika matumizi mbalimbali ikiwemo kufua,kunywesha mifugo.
Maji ni uhai kwa binadamu na viumbe hai pamoja na mimea,hivyo basi serikali kama ipo katika mipango ya kupeleka huduma ya maji safi katika maeneo hayo amabayo hayapati huduma hizo ni vyema ikaharakisha ili kunusuru afya zao.
Post a Comment
karibu kwa maoni