Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Venance Msafiri amewataka wanachama
ambao kwa sasa wanafanya uhaguzi kuchagua viongozi waadilfu ili kuweza kuendeleza ushirika huo.
Aidha amesema kwa kiongozi yeyote atakayebainika kutoa rushwa ili achaguliwe ataondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi na kuchuuliwa hatua za kinidhamu.
Msafiri ametoa wito huo wakati alipokuwa akizuingumza na kituo hiki ofisini kwake ambapo amesema kuwa zoezi la uchaguzi katika vyama mbalimbali linaendelea na litakamilika mwezi wa kwanza kwa ajili ya kupisha uchaguzi mkuu viongozi ngazi ya mkoa.
Vyama vya ushirika mkoa wa Manyara vinaendelea na chaguzi mbalimbali mpaka april mwakani watakapofanya uchaguzi mkuu mkoa, na viongozi watakaopatikana wataongoza kwa miaka sita kwa awamu mbili.
Kwa upande mwingine Mrajisi Venance Msafiri amesema kwa sasa wameshasajii vyama vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa ,Manyara na kuwasisitiza vijana wengine kujiunga na vyama vya ushirika ili kupata fursa mbalimbali ambazo zitawasaidia kuwakomboa kiuchumi.
Mbali na vijana mrajisi pia ameeleza wamesajili vyama mbali mbali vya wakulima,wafugaji na viwanda ili kuunga mkono serikali ya awamu ya tano inayosisitiza Tanzania ya Viwanda.
Msafiri amesema mpaka kufikia oktoba 30 mwaka huu wamesajili vyama vya ushirika 249 katika mkoa wa Manyara.
Post a Comment
karibu kwa maoni