Na
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
TANZANIA
imezidi kupata neema kutoka Jumuiya ya Kimataifa ambapo Novemba 2, 2017, Umoja
wa Ulaya (EU) umeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 50, takriban Shilingi
bilioni 130 kwa ajili ya kufadhili Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini
unaoendeshwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Mkataba
wa Makubaliano hayo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu na
Mlipaji Mkuu wa Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na
Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw.
Neven Mimica.
Msaada
huo umelenga kuwasaidia raia wa Tanzania kufikiwa na huduma nafuu ya nishati ya
umeme kwa kupanua uwezo wa gridi ya Taifa pamoja na mtandao wa usambazaji
umeme.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James ameushukuru Umoja wa Ulaya
kwa msaada huo mkubwa utakaoiwezesha nchi kuwa na umeme wa uhakika
utakaochangia ukuaji wa uchumi wa nchi na maendeleo ya watu wake.
“Umoja wa ulaya ni wadau wetu
muhimu wa maendeleo kutokana na misaada muhimu na mikubwa wanayotupatia, na
kusadia agenda yetu ya maendeleo” alisema Bw. James
Alisema
kuwa kiasi cha msaada wa Euro milioni 50 kilichotolewa na Umoja huo bila
masharti yoyote si kidogo, na kwamba kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji
wa nishati ya umeme utakaochangia kuimarika kwa sekta ya viwanda itakayochochea
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Bw.
Doto James alisema kuwa tangu Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini REA
uanze miaka 9 iliyopita, idadi ya vijiji vilivyounganishiwa umeme imeongezeka
kutoka vijiji 400 mwaka 2008 hadi kufikia vijiji 4395 hivi sasa.
Alisema
kuwa ni matarajio ya Serikali kwamba ifikapo mwaka 2020, vijiji vyote 12,000 hapa
nchini vitakuwa vimeunganishwa na nishati hiyo hivyo kuchochea shughuli za
uzalishaji viwandani na kiuchumi kwa wananchi, vitaimarika.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Umoja wa
Ulaya (EU) Bw. Neven Mimica, amesema kuwa msaada huo wa Euro milioni 50
wanaoutoa ni sehemu ya msaada wa Euro milioni 207 ambazo wanachama wengine wa
Umoja huo, ikiwemo Sweden, Uingereza, Norway na Benki ya Dunia, watatoa kufanikisha
mradi huo wa usambazaji umeme vijijini kupitia REA.
“Nguvu
hizi za pamoja zitaviwezesha takriban vijiji 3,600 vilivyoko maeneo mbalimbali
ya nchi ambapo watu zaidi ya milioni 1 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo”
Alisema Bw. Mimica
Alisema
hatua hiyo itachangia kuimarika kwa ubora wa maisha ya wananchi wa Tanzania,
kuimarika kwa sekta za afya, elimu na kuleta faida za kijamii na kiuchumi zinazoonekana
kwao moja kwa moja hususan wanawake na watoto.
Misaada
ya Umoja wa Ulaya kwa Tanzania imejikita katika Nyanja tatu za Utawala bora,
Umeme na Kilimo endelevu ambapo Umoja huo kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF)
umetenga kiasi cha Euro milioni 626 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014-2020
Post a Comment
karibu kwa maoni