0
Mwanariadha aliyekuwa tegemeo kubwa katika kuiwakilisha Tanzania kwenye Mashinadano ya dunia Ismail Juma Aliefariki jana kwa ajali ya piki piki atazikwa kesho nyumbani kwao kijiji cha Gendi mjini Babati. 
Tasnia ya mchezo wa Riadha imepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mchezaji wa mchezo  huo Isamil Juma Gallet ambae amefariki jana alihamisi kwa ajali  ya pikipiki kugongana na gari aina ya Fuso tukio ambalo  lilitokea  katika kijiji cha Nangara
Wilayani Babati Mkoani hapa.

Akiongea na WALTER BLOG Nyumbani kwao  marehemu Baba mzazi wa mchezaji huyo Juma Mohammed Gallet alisema siku ya Alhamisi majira ya saa kumi kamili za jioni marehemu alienda Mjini Babati kuchukua nafaka aina ya mahindi ambapo wakati wa kurudi ndipo  akapata ajali hiyo na kusababisha kifo chake na mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospital ya Wilaya ya Babati Mrara.

"Ismail alienda kuchukua mahindi Babati saa  kumi za jioni alaipokuwa anarudi akakutana na gari ndipo akakumbwa na ajali hiyo na kusababisha kifo chake" Alisema Gallet.

Kwa upande wa Mwenyewekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa
Manyara Safari Ingi alisema wamepokea taarifa za kifo cha Ismail Juma kwa
Mshtuko makubwa sana ukiangalia alikuwa ni mwanaridha ambae alikuwa anategemewa
sana kuja kuiletea Taifa Eshima.

"Chama cha Riadha Manyara imepokea kwa masikitiko makubwa sana habari ya kifo cha Ismail Juma kijana ambae tulikuwa tunamtegemea kwa Olimpiki ya 2020 ndio angeweza kutuletea medali na kama tunavyojua Mwaka huu mwezi wa tisa Ismail Juma alivunja rekodi ya taifa kwa kukimbia dakika 59 sekunde 30 katika mbio za Nusu Marathon ambazo ni 21 kilomita kwa hiyo Mategemeo ya WaTanzania ilikuwa  ni kwamba tunamuandaa kuja kuwa shujaa ambae angeweza kuiketea heshima nchi hii lakini Mungu kaamua kumchukua
tumepokea taarifa za kifo chake kwa mshituko mkubwa  sana binafsi
sikuamini lakini ndo naamini sasa." Alisema Ingi.

Kocha wa Mwanariadha huyo Denis Malley Alisema nimepokea taarifa hizi kwa uchungu sana kuliko mtu  yeyote kwani ukiangalia Mwaka huu ndio Ismail alianza kuwa Kwenye soko  la dunia  nimeumia sana sana sina la kusema.

Marehemu Ismail Juma alikuwa kati ya wanariadha ambao majina yao yamewasilishwa ofisi za kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) tayari kwa kuwakilisha nchi katika Mashindano ya jumuiya ya Madola(2018 Gold Coast Commonwealth Games) na Kwa mujibu wa Baba wa Marehemu mazishi ya Mwanariadha huyo yanatarajiwa kufanyika leo jumamosi huko kijijini kwao Gendi Wilayani Babati Mkoani Hapa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top