Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Alexander Mnyeti amekaribishwa rasmi katika mkoa wa Manyara tayari kwa kuanza kutumiika kama mkuu wa mkoa wa Manyara.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Dk Joel Nkaya Bendera ambaye kwa sasa amestaafu amemtaka Mnyeti kuundeleza mkoa wa Manyara katika maendeleo kwa kuhamasisha wananchi kuendeleza kilimo cha kisasa ambacho ndicho kiinua mgongo ndani ya mkoa.
Amesema mkoa huu ndio unaoongoza katika makusanyo ya mapato kanda ya kaskazini kwa na mkoa haujawahi kufanya vibaya hivyo lkwa sasas ni kuweka mkazo zaidi ili watu waendelee kujituma.
ULINZI NA USALAMA
Kuhusu ulinzi na Usalama Dr.Bendera amesema kwa sasa hali ya mkoa ipo shwari kabisa baada ya kumaliza migogoro iliyokuweopo kwa muda mrefu katika wilaya ya Kiteto na kijiji cha Kiru
wilayni Babati juu ya wakulima na wafugaji katika kugombea mashamba.
wilayni Babati juu ya wakulima na wafugaji katika kugombea mashamba.
Kususu siasa Bendera amemtaka Mnyeti kuhakikisha Chama cha mapinduzi kinashinda katika chaguzi mbaliombali ndani ya mkoa wa Manyara.
Post a Comment
karibu kwa maoni