Kikosi
cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho
Alhamisi kwenda nchini Benin kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa wa
kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Fifa.
Taifa
Stars inakwenda Benin bila ya nahodha wake, Mbwana Ally Samatta ambaye
ameumia goti na atatakiwa kukaa nje kwa wiki sita akipata matibabu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Alfred Lucas alisema kuwa wachezaji wote wameshaingia kambini
kasoro nahodha, Mbwana Samatta ambaye ni majeruhi pamoja na Abdi Banda.
“Kikosi
cha timu yetu ya taifa kinatarajia kuondoka hapa keshokutwa (kesho),
Novemba 9, alfajiri kwenda Benin kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya
kirafiki na kitakapofika rasmi kesho yake kitaendelea na programu yake
mazoezi huko Benin,” alisema Lucas.
Post a Comment
karibu kwa maoni