Wachezaji watatu wa mpira wa vikapu
wa ligi ya vyuo nchini Marekani wamekamatwa nchini China kwa wizi wa
dukani kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Wachezaji hao
wa chuo kikuu cha California, mjini Los Angeles UCLA walikamatwa katika
duka la Louis Vuitton kulingana na chombo cha habari cha ESPN.Klabu hiyo ya UCLA iko nchini China kushiriki katika mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya timu nyengine ya Marekani Georgia Tech.
Watatu hao walikamatwa siku ya Jumanne , siku moja kabla ya ziara ya rais Donald Trump nchini China.
Wachezaji wanaozuiliwa katika mji wa Hangzhou ni Cody Riley, LiAngelo Ball na Jalen Hill kulingana na gazeti la Los Angeles Times na ESPN ikitaja duru ambazo hazikutajwa.
''Tunaelewa kuhusu hali iliowapata wachezaji wa UCLA mjini Hangzhou, China'', alisema msemaji wa klabu hiyo Shana Wilson katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya Marekani.
''Chuo hicho kinashirikiana kikamilifu na mamlaka husika kuhusu swala hilo na hatuna maelezo zaidi wakati huu''.
Wanafunzi watatu wa Georgia pia walihojiwa lakini hawakukamatwa , Chuo hicho kilisema kwa vyombo hivyo vya habari.
Klabu hizo mbili ziko China ikiwa ni miongoni mwa malengo yao ya Pac-12 Global initiative ya kupija jeki uwepo wao na uzoefu wa kibinafsi wa wachezaji.
Mechi hiyo ya kufungua msimu siku ya Ijumaa mjini Shanghai inafadhiliwa na Alibaba.
Post a Comment
karibu kwa maoni