0




Siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender
Mnyeti  kumuamuru mkurugenzi  wa Halmashauri wa mji wa Babati kufuta alama
za X zilizokuwa zimepigwa katika nyumba 
eneo la Sinai kata ya Maisaka na Kwere kata ya Babati mbunge  Pauline Gekul ameliunga mkono.
Hata hivyo mheshimiwa Gekul amekiri kuwa wananchi wanafanya
makosa kwa kujenga bila kuwa na vibali pamoja na kuvamia maeneo ya wazi ambayo
kwa mujibu wa mipango miji yanakatazwa kufanywa shughuli yoyote.








Mbunge huyo kwa tiketi ya chama cha demokrasia na Maendeleo
CHADEMA amesema yeye hakuwahi  kushauri
kupitisha wananchi kubolewa nyumba zao na alishawahi kuzungumza  katika ziara zake kuwa hilo litajadiliwa
katika vikao vya madiwani.
Mbali na kumuunga mkono mkuu wa mkoa kwa kuchukua maamuzi hayo
ambayo yamewapa faraja na matumaini wakazi ambao walitaka kubomolewa nyumba zao
huku wengine wakilazwa hospitali kwa mshtuko amesema alipaswa kuwashirikisha
viongozi wa kata husika na mtaa katika kutoa maamuzi hayo.
Akimweleza mkuu wa mkoa kwanini wameamua kubomoa nyumba hizo
Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alisema  Nyumba hizo zimejengwa  kiholela bila kufuata taratibu zinazohitajika
na mipango miji huku mkuu wa mkoa Alexender Mnyeti akionekana kukerwa na
kitendo hicho na kumtolea karipio kali mkurugenzi mbele ya umati wa watu
waliokusanyika kupata majibu kuhusu hatma ya nyumba zao na viwanja.
Ina maana kuwa Nyumba hizo zingebolewa  watu zaidi ya 400 wangekosa  mahali pa kuishi kwani wengi wao walikuwa
wakiishi nyumba za kupanga na ndio ilikuwa mara yao ya kwanza  kumiliki nyumba.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top