Kundi moja la wanaharakati wa haki
za wanyama nchini limekosoa uchomaji wa kuku 6,400 walioingizwa
nchini humo kutoka Kenya kinyume na sheria ili kukabiliana na mlipuko
wa ugonjwa wa homa ya ndege.
Kuku hao walichomwa na maafisa wa
wizara ya mifugo na uvuvi wakishirikiana na maafisa wa usalama baada ya
kukamatwa katika mpaka wa Namanga siku ya Jumatatu usiku.Mfanyiabiashara Mary Matia,23, aliwaingiza kuku hao wenye thamani ya $5000 kutoka Kenya na aliangalia kwa uchungu mkubwa na kutoamini wakati vifaranga hao walipochomwa , alisema mwandishi wa BBC Balthazar Nduwayezu kutoka mji wa Namanga.
Tanzania ilipiga marufuku uingizaji wa kuku yapata muongo moja uliopita kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ndege katika eneo la Afrika mshariki.
Post a Comment
karibu kwa maoni